Baada ya kusimama mjini Cairo Blinken ataelekea Jerusalem siku ya Jumatatu, ambako serikali mpya ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ya mrengo wa kulia imezua wasiwasi ndani na nje ya nchi hiyo kuhusu mustakabali wa maadili yasiyo ya kidini ya Israel, kuvuruga uhusiano wa kikabila na kukwamisha mazungumzo ya amani na Wapalestina.
Pia kumekuwa na msururu wa ghasia mbaya katika siku za hivi karibuni, na hivyo kuzidisha hofu kwamba ghasia ambazo tayari zimeshamiri zitaongezeka zaidi.
Mtu aliyekuwa na silaha raia wa Palestina aliwaua watu saba katika shambulizi nje ya sinagogi la Jerusalem siku ya Ijumaa. Lilikuwa shambulio baya zaidi kama hilo dhidi ya Waisraeli katika eneo la Jerusalem tangu mwaka 2008 na lilifuatia shambulio baya la Israel katika mji unaokaliwa kimabavu wa Ukingo wa Magharibi wa Jenin siku ya Alhamisi, shambulio baya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka kadhaa.