Waziri wa fedha wa Marekani, Janet Yellen, anaelekea Senegal, Zambia na Afrika Kusini wiki hii kujadili kupanua ushirikiano wa biashara, uwekezaji na azma ya Marekani katika uchumi wa Afrika.
Ziara hii inafanyika baada ya ahadi kutoka kwa rais wa Marekani, Joe Biden, wakati wa mkutano wa Marekani na viongozi wa Afrika mwezi uliopita kwamba yeye na mawaziri wake watatembelea Afrika kwa mwaka huu wa 2023.
Maafisa waandamizi wa wizara ya fedha wanasisitiza kwamba madhumuni ya ziara hiyo ni kubadilishana uzowefu na serekali za Afrika, sekta binafsi, wajasiriamali na vijana, pamoja na kupanua uhusiano wa kiuchumi baina ya Marekani na Afrika, ikiwa ni kuangazia pia fursa mpya za biashara na uwekezaji.
Akiwa katika mataifa hayo atafanya shughuli mbalimbali za kiuchumi na masuala ya urithi wa dunia chini ya UNESCO.