Waziri mkuu wa Pakistan, hatimaye atarajiwa kufika mahakamani

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistani, Imran Khan

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan, alitarajiwa kufikishwa mahakamani Jumamosi kujibu mashtaka ya kuuza kinyume cha sheria zawadi za serikali alizopokea wakati wa miaka yake minne alipokuwa madarakani.

Hatimaye uamuzi wa Khan kufika mahakamani umekuja baada ya mahakama kuu ya Islamabad siku ya Ijumaa kufuta amri ya kukamatwa ambayo mahakama ya chini ilitoa mapema mwezi huu.

Ilifanywa hivyo baada ya kushindwa kufika mahakamani katika tarehe kadhaa za karibuni alizopangiwa na mahakama.

Wakati huo huo, maelfu ya maafisa wa polisi walitumwa ndani na karibu na jengo la mahakama katika mji mkuu wa Pakistani kabla ya kuonekana kwa Khan baada ya mwanasiasa huyo wa upinzani kueleza uwepo wa vitisho kwa maisha yake.

Mapigano kati ya wafuasi wa Khan na vikosi vya usalama yalizuka mapema wiki hii nje ya makazi yake mjini Lahore, mji mkuu wa Punjab.