Waziri mkuu wa Japan anataka kukutana na Trump

Waziri mkuu wa Japan Shigeru Ishiba Nov 29, 2024

Waziri mkuu wa Japan Shigeru Ishiba, amesema leo Jumanne kwamba anataka kuimarisha ushirikiano wa nchi yake na Marekani, wakati anapanga kukutana mapema na rais mteule Donald Trump.

Japan ni Jirani wa China na Korea kaskazini yenye silaha za nyuklia na ambayo imekuwa ikiimarisha ushirikiano wake na Russia.

Ishiba ameambia waandishi wa habari kwamba ni muhimu kuimarisha zaidi uhusiano kati ya Japan na Marekani na kuwa na msimamo mmoja kuhusu maswala yanayoendelea kaskazini mashariki mwa Asia.

Ishiba amekuwa ofisini tangu mwezi Oktoba.

Amesema baraza la mawaziri la Japan litaidhinisha bajeti ya mwaka ujao hapo Desemba 27. Bajeti hiyo itaanza kutumiaka mwezi April.