Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliiambia Fox News Alhamisi kwamba Israel haina nia ya kuiteka, kuikalia au kuitawala Gaza.
Kiongozi wa Israel pia hana nia ya kusitisha mapigano. "sitisho la mapigano na Hamas linamaanisha kusalimu amri," aliongeza.
Mapema wiki hii, kiongozi huyo wa Israel alisema kuwa Israel itasimamia usalama wa Gaza, bila kutoa maelezo jinsi itakavyokuwa.
Siku ya Alhamisi, Netanyahu aliiambia Fox kwamba "kikosi cha kuaminika" kinapaswa kuwekwa Gaza ili kuzuia vitisho vya wanamgambo, kama vile mashambulizi ya Hamas nchini Israel.