Waziri Mkuu wa India anawahimiza wananchi wake kuchomwa chanjo dhidi ya COVID-19

Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi

Narendra Modi aliwasihi pia kuamini sayansi na wanasayansi katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona ambavyo vimeongezeka nchini India. Wizara ya afya ya India hapo Jumapili iliripoti zaidi ya kesi mpya 50,000 za COVID-19 na zaidi ya vifo 1,200

Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, alisema Jumapili katika matangazo yake ya kila mwezi kwamba tishio la COVID-19 bado lipo na tunapaswa kuzingatia chanjo, pamoja na kanuni za COVID-19.

Modi aliwashawishi wananchi wa India kupata chanjo na kuacha kusita kutopata chanjo yeyote. Aliwasihi pia kuamini sayansi na wanasayansi katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona, ambavyo vimeongezeka nchini India. Wizara ya afya ya India hapo Jumapili iliripoti zaidi ya kesi mpya 50,000 za COVID-19 na zaidi ya vifo 1,200.

Kulingana na kitengo kinachofuatilia kesi za virusi vya Corona cha John Hopkins cha Marekani, India ni nchi ya pili baada ya Marekani katika idadi ya kesi za virusi vya Corona lakini maafisa wa afya wanaonya kwamba idadi ya kesi za India zinaweza kuwa ndogo kuliko uhalisia.