Waziri Mkuu mpya wa Uingereza amekutana na baraza lake la mawaziri

Waziri Mkuu mpya wa Uingereza, Keir Starmer na kiongozi wa chama cha Labour akiwa nje ya jengo la 10 Downing Street in London on July 5, 2024.

Kazi ya mabadiliko inaanza mara moja, Starmer alisema baada ya kuthibitishwa kama Waziri Mkuu na Mfalme Charles III wa London

Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Keir Starmer leo Jumamosi alianza siku yake ya kwanza madarakani kwa mkutano wa baraza lake la mawaziri baada ya ushindi wa chama chake cha Labour uliomaliza miaka 14 ya utawala wa Conservative.

Starmer alifanya mkutano wake wa kwanza wa baraza la mawaziri saa tano asubuhi kwa saa za London, na waziri wa kwanza mwanamke wa fedha wa Uingereza Rachel Reeves na waziri mpya wa mambo ya nje David Lammy.

Kiongozi wa Labour alitumia saa zake za kwanza huko Downing Street siku ya Ijumaa akiteua timu yake ya mawaziri, saa kadhaa baada ya kukipatia chama chake cha mrengo wa kati -kushoto kurudi madarakani kwa wingi wa viti 174 katika bunge la Uingereza.

Kazi ya mabadiliko inaanza mara moja, Starmer alisema Ijumaa muda mfupi baada ya kuthibitishwa kama Waziri Mkuu na Mfalme Charles III na umati wa watu waliopeperusha bendera ya chama cha Labor waliomkaribisha Downing Street.