Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken ataondoka Alhamisi kuelekea Mashariki ya Kati, ikiwa ni pamoja na kusimama nchini Israel, huku Marekani ikiendelea na mashauriano ya kidiplomasia kuhusu mzozo wa Israel na Gaza, afisa mwandamizi wa Marekani amesema Jumatano.
Afisa huyo, akiwaeleza waandishi wa habari kwa masharti ya kutotajwa jina, amesema mjumbe wa kidiplomasia wa Marekani, Amos Hochstein, pia atasafiri mpaka Israel, kujaribu kutuliza mivutano kati ya Israel na Hezbollah.
Waziri Blinken, anaondoka leo usiku ambapo atakuwa na vituo vya miji mikuu kadhaa, pamoja na Israeli,” afisa huyo amesema bila ya kutoa maelezo zaidi.
Rais wa Marekani Joe Biden alizungumza kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, hivi karibuni akifanya kazi ya kuboresha ufikiwaji wa Gaza kwa ajili ya misaada ya kibinadamu na kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas.