Waziri Blinken asema mauaji ya Yahya Sinwar yanatoa fursa halisi ya kufikia makubaliano ya kuwaachilia mateka

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alipokfanya ziara Lagos Nigeria Januari 2 ,2024(REUTERS).

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema Jumatano kwamba mauaji ya Israel ya kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar yanatoa fursa halisi ya kufikia makubaliano ya kuwaachilia mateka

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema Jumatano kwamba mauaji ya Israel ya kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar yanatoa fursa halisi ya kufikia makubaliano ya kuwaachilia mateka waliosalia ambao bado wanashikiliwa na kundi la wanamgambo katika Ukanda wa Gaza.


Akizungumza na waandishi wa habari mjini Tel Aviv kabla ya kuelekea Saudi Arabia, Blinken alisema Israel imepata mafanikio kadhaa katika vita dhidi ya Hamas, ikiwa ni pamoja na kupunguza uwezo wa kijeshi wa kundi hilo.


Blinken alikutana na kiongozi wa Saudia Mohammed bin Salman kwa saa moja mjini Riyadh na anaelekea Qatar na kisha Uingereza kwa mazungumzo zaidi na maafisa ili kujaribu kusimamisha mapigano ya Israel na Hamas huko Gaza na Hezbollah nchini Lebanon. Makundi yote mawili ya wanamgambo yanaungwa mkono kijeshi na kifedha na Iran.