Waziri mkuu wa Somalia amemsimamisha kazi waziri wa mambo ya nje kwa kuagiza usafirishaji wa mkaa kutoka nchini humo hadi Oman, hatua inayokiuka vikwazo vya kimataifa.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa lilipiga marufuku uuzaji wa bidhaa kwa Oman mwongo mmoja uliopita, ili kupunguza ufadhili kwa kundi la wapiganaji wa kiislamu la Al-shabaab, linalopigana na serikali ya Somalia.
Ofisi ya waziri mkuu Mohamed Hussein Roble, imesema kwamba kando na kumsimamisha kazi Abdisaid Muse Ali, ameamuru kufanyika ukaguzi wa kina na uchunguzi kuhusu usafirishaji wa mkaa kutoka Somalia hadi Oman.
Juhudi za kupata taarifa kutoka kwa wizara ya mambo ya nje hazijafanikiwa.
Hakuna taarifa zaidi kuhusu kiasi cha mkaa uliokuwa ukisafirishwa kutoka Somalia kuelekea Oman.