Shirika la habari la Reuters linamenukuu taarifa ya polisi iliyoeleza kwamba shambulizi hilo, ambalo lilishababisha vifo vya dereva wa basi na abiria, lilitekelezwa na National Liberation Front (FLN), tawi la waasi la Movement for Democratic Change (MRCD) linalopinga serikali.
Polisi wamesema wanawasaka watu waliovamia basi hilo katika barabara ya Nyambage-Rusizi, katika msitu wa Nyungwe.
Serikali inasema FLN ilianzisha mashambulizi kutoka eneo la msitu wa Nyungwe karibu na mpaka wa Burundi mwaka wa 2018.
Mwezi Aprili, serikali ya Rwanda iliidhinisha kifungo cha miaka 25 jela kwa Paul Rusesabagina, ambaye alionyeshwa kwenye sinema ya "Hotel Rwanda" akiwahifadhi mamia ya watu wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994, kwa kuhusika kwake na MRCD.
Alihukumiwa mwezi Septemba mwaka jana, baada ya kupatikana na hatia kwa mashtaka nane ya ugaidi, ambayo ameyakanusha.