Katsina ni moja ya majimbo kadhaa kaskazini magharibi na katikati mwa Nigeria yanayokumbwa na mashambulizi ya magenge ya uhalifu, yanayojulikana kama majambazi, ambao huvamia vijiji, kuua na kuteka nyara wakazi pamoja na kuchoma nyumba zao baada ya kuwapora.
Magenge hayo, ambayo yana ngome katika misitu mikubwa inayozunguka majimbo ya Zamfara, Katsina, Kaduna na Niger, yamekuwa mashuhuri kwa utekaji nyara mkubwa wa wanafunzi wa shule katika miaka ya hivi karibuni.
Watu kadhaa wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki walishambulia kijiji cha Kusa katika wilaya ya Musawa nyakati za usiku siku ya Jumapili na kuwafyatulia risasi watoto wa shule wakisherekea Maulidi katika kijiji hicho, kiongozi wa wilaya ya Musawa Habibu Abdulkadir ameiambia AFP kwa njia ya simu.