Katika wagonjwa waliopatikana ni mwanaume mtanzania mwenye umri wa miaka 40 aliyesafiri nchi za Uswisi, Denmark na Ufaransa kuanzia Machi 5 hadi 13 mwaka huu na kurejea nchini Machi 14.
Mwingine ni Mwanaume mtanzania mwenye umri wa miaka 40 pia ambaye alisafiri Afrika Kusini kati ya tarehe 14 Machi hadi 16 na kurejea nchi Machi 17 usiku.
Wahusika hao wote wametengwa na hali zao zinaendelea vizuri huku juhudi za kufuatilia watu walio karibu na wagonjwa waliothibitika kuwa na COVID 19 zinaendelea ambapo hadi sasa idadi ya watu 46 wanafuatiliwa Jijini Arusha na watu 66 wanafuatiliwa jijini Dar es Salaam.
Taarifa hizi zimetolewa Alhamisi na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu juu ya mwenendo wa Maambukizi ya Virusi vya Corona COVID 19 nchini Tanzania katika kipindi cha saa 24 zilizopita.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Tanzania.