Watu wanne wafariki katika mkanyagano nchini Kenya

Ramani ya Kenya

Wanawake wanne walifariki leo Ijumaa katika mkanyagano magharibi mwa Kenya baada ya umati wa watu kutaharuki walipodhani kuwa chai iliyomwagika kwenye moto ni gesi ya kutoa machozi, polisi wamesema.

Wanawake wanne walifariki leo Ijumaa katika mkanyagano magharibi mwa Kenya baada ya umati wa watu kutaharuki walipodhani kuwa chai iliyomwagika kwenye moto ni gesi ya kutoa machozi, polisi wamesema.

Tukio katika mji wa Kericho lilitokea nje ya uwanja wa michezo ambako Rais William Ruto alitarajiwa kutoa hotuba ya kitaifa saa kadhaa baadaye.

Mwanamke aliyekuwa anauza chai aliimwaga kwenye moto kwa bahati mbaya, wakati watu walikuwa wakisubiri nyakati za alfajiri kuingia uwanjani.

Sherehe za kuadhimisha siku ya mashujaa ziliendelea kama ilivyopangwa kwenye uwanja wenye uwezo wa kupokea watu 10,000, ikiwemo hotuba ya Ruto.