Watu walioshambulia bunge la Marekani kufunguliwa mashitaka

Watu wakiwa kwenye bustani karibu na jengo la bunge ya Marekani

Mweyekiti wa kamati ya bunge la Marekani inayochunguza shambulizi la Januari 6, 2021 kwenye majengo  ya bunge, Bennie Thompson amesema kwamba wanapanga kuwasilisha ombi kwa wizara ya sheria  kupendekeza kushtakiwa kwa waliohusika.

Hata hivyo Thomson hakufichua iwapo rais wa zamani wa Marekani Donald Trump atakuwa miongoni mwa watakaofunguliwa mashitaka. Amesema kwamba kamati yake ya watu 9 ilikuwa inakamilisha mapendekezo yake wakati ikimaliza uchunguzi kuhusu uvamizi huo uliyofanywa na takriban watu 2,000 wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Trump, wakiwa na nia ya kuvuruga kikao cha bunge cha kuidhinisha ushindi wa Joe Biden kwenye uchaguzi wa rais wa 2020.

Wakati akihutubia wanahabari kwenye majengo ya bunge, Thomson amesema kwamba kuna nakala tofauti itakayowasilisha kwa wizara ya sheria kutokana na uchunguzi wa kamati yake.