Watu waliojihami wazuia uchaguzi wa waziri mkuu Libya

Majengo ya bunge mjini Tripoli

Kura hiyo ilikuwa ya kuziba nafasi ya Abdullah al-Thani ambaye alijiuzulu mwanzoni mwa mwezi huu.
Watu wenye silaha walilishambulia bunge la Libya wakifyatua risasi na kusababisha wabunge kuahirisha kura ya kumchagua waziri mkuu mpya nchini humo.

Maafisa wa Libya wanasema watu hao wenye silaha walivunja mlango na kuingia ndani ya ofisi za jengo la katibu mkuu wa bunge mjini Tripoli Jumanne na kufyatua risasi hewani.

Shirika la habari la Reuters liliripoti kuwa watu kadhaa walijeruhiwa katika ufyatyuaji risasi huo. Shirika hilo linamnukuu msemaji wa bunge, Omar Hmeidan, akisema watu hao wenye silaha walikuwa na uhusiano na mmoja wa wagombea aliyeshindwa kwenye nafasi ya waziri mkuu.

Kura hiyo ilikuwa ya kuziba nafasi ya Abdullah al-Thani ambaye alijiuzulu mwanzoni mwa mwezi huu.

Duru ya pili wa uchaguzi huo uliovurugika ilikuwa kati wagombea wawili, mfanyabiashara Ahmed Matiq na profesa wa masuala ya kisiasa, Omar al-Hassi