Watu nane wameuwawa na mlipuko wa bomu Somalia.

Ramani ya somalia

Maafisa kusinimagharibi mwa somalia wanasema mlipuko wa bomu umewauwa watu nane waliokuwa wanasafiri kwa basi dogo.

Maafisa kusinimagharibi mwa somalia wanasema mlipuko wa bomu umewauwa watu nane waliokuwa wanasafiri kwa basi dogo.

Takriban watu wengine 13 wamejeruhiwa katika shambulii hilo la bomu lililotokea jumanne usiku katika eneo ambalo serikali ya mpito ya Somalia imekuwa ikipigana na kundi la wanamgambo la al- Shabab .

Radio moja ya ndani –Garowe, imetangaza katika mtandao wake wa tovuti kwamba basi hilo dogo la abiria lilikuwa linakimbia mapigano yenye maafa makubwa baina ya wanamgambo wa kiislamu wenye msimamo mkali na majeshi yanayounga mkono serikali .

Kundi la al- Sshaba linadhibiti eneo kubwa la kusini na kati ya somalia.

Serikali hivi karibuni ilianzisha mashambulizi yenye lengo la kutimua kundi hilo la wanamgambo.

Kundi la al- Shabab limekuwa likifanya mashambulizi mengi ya mabomu nchini somalia ikiwemo ya kujitoa muhanga na yale ya kutegwa ardhini jambo ambalo limepelekea mauaji makubwa , majeruhi na hata kuzorotesha maendeleo ya nchi hiyo.