Hali ya ukame inaathiri jamii za wafugaji na wakulima kote kusini na kusini-mashariki mwa Ethiopia, kusini-mashariki na kaskazini mwa Kenya, na kusini-kati mwa Somalia.
Watu katika eneo ikiwa ni pamoja na Somalia, Ethiopia na Kenya wanakabiliwa na hali mbaya sana ya ukame uliorekodiwa tangu 1981, shirika hilo liliripoti Jumanne, likitoa wito wa msaada wa haraka ili kuepusha janga kubwa la kibinadamu.
Hali ya ukame inaathiri jamii za wafugaji na wakulima kote kusini na kusini-mashariki mwa Ethiopia, kusini-mashariki na kaskazini mwa Kenya, na kusini-kati mwa Somalia. Viwango vya utapiamlo viko juu katika eneo hilo.
WFP imesema inahitaji dola milioni 327 kushughulikia mahitaji ya dharura ya watu milioni 4.5 katika kipindi cha miezi sita ijayo na kuzisaidia jamii kuhimili majanga makubwa ya hali ya hewa.