Mamlaka ya kukabiliana na majanga nchini Afghanistan imesema kwamba watu 31 wamefariki, 74 kujeruhiwa na 41 hawajulikani walipo kutokana na mafuriko katikati mwa nchi hiyo.
Msemaji wa mamlaka hiyo amewaambia waandishi wa habari kwamba maafa makubwa yalitokea katika mkoa wa Wardak, katikati mwa Afghanistan kutokana na mvua kubwa na mafuriko, katika muda wa siku tatu zilizopita.
Video inayoonyesha mfuriko hayo imetolewa na shirika la habari la China na hivyo VOA haiwezi kuthibitisha uhalali wa video hiyo.
Mamlaka nchini Afghanistan wamesema kwamba juhudi za uokoaji zinaendelea.
Idhara ya majanga nchini Afghanistan hata hivyo imesema kwamba watu 214 wamefariki, 320 kujeruhiwa na ng’ombe 3800 kufa.