“Tunaweza pia kuthibitisha walau mlipuko mmoja mwingine umetokea kwenye au karibu na hoteli ya Baron, mwendo mfupi kutoka mlango wa Abbey,” msemaji wa Pentagon John Kirby ameandika kwenye Twitter.
Maelfu ya watu wamefurika kwenye uwanja wa ndege katika siku za karibuni wakijaribu kuondoka nchini humo kufuatia Taliban kuchukua udhibiti wa Afghanistan.
Chanzo cha ngazi ya juu cha Taliban kimeithibitishia VOA kwamba mlipuaji mmoja wa kujitoa mhanga alijilipua nje ya uwanja huo ambako idadi kubwa ya watu, wakiwemo wanawake walikuwa wamekaa. Hakuna aliyedai kuhusika na mlipuko.
Serikali za Magharibi zilionya mapema Alhamisi juu ya tishio ya shambulizi la kigaidi kwenye uwanja wa ndege na kusema wale waliokusanyika katika eneo hilo wakitaka kuondoka nchini humo ni vyema wahamie eneo salama.
“Kwasababu tya vitisho vya usalama nje ya milango ya uwanja wa ndege wa Kabul, tunawashauri raia wa Marekani kuepuka kusafiri kwenda uwanja wa ndege na kuepuka kuwepo kwenue milango ya uwanjani hapo mpaka watakapopata maelekezo maalum kutoka mwakilishi wa serikali ya Marekani,” ubalozi wa Marekani mjini Kabula umesema katika taarifa. “Raia wa Marekani ambao walikuwa katika maeneo ya milango ya Abbey, East au North ni vyema waondoke haraka sana.”
Watu kadhaa waliojeruhiwa waliwasili katika hospitali ya dharura ya Kabul, inayoendeshwa na shirika lisilo la kiserikali ambayo linawahudumia waathirika wa vita na mabomu ya kutegwa ardhini. Vyombo vya habari vya Afghansitan vimetweet picha za raia wakiwasafirisha watu waliojeruhiwa kwa kutumia matoroli.
Waziri wa majeshi ya ulinzi ya Uingereza, James Heappey aliiambia radiao ya BBC mapema, “hivi sasa kuna habari za uhakika kabisa juu ya kutokea kwa shambulizi.”
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken alirejea kusema jana kwamba Marekani inaona uwezekano wa tishio kutoka kwa makundi yenye uhusiano na Islamic State yanayojihusisha nchini Afghanistan.
Marekani imeahidi kuendelea na juhudi za kuwaondoa raia wa Marekani, wakazi wa kudumu wa Marekani, washirika na raia wengine wa Afghanistan ambao wako katika hatari, hata kama muda uliowekwa wa kuondoka kwa wanajeshai wa Marekani mwisho wa mwezi utakuwa umepita.