Ofisi ya waziri mkuu haikutangaza idadi kamili ya vifo katika eneo la Karamoja.
Zaidi ya watu nusu milioni wanakabiliwa na njaa huko Karamoja, ni asilimia 40 ya wakazi wa eneo hilo la vijijini lililotelekezwa, lililotaabika kwa muda mrefu ambalo linapatikana kati ya Sudan Kusini na Kenya.
Eneo hilo lilikumbwa na ukame mbaya mwaka jana na kushuhudia mafuriko na maporomoko ya ardhi.
Kulikuwa pia nzige na uvamizi wa wezi wa mifugo wenye silaha nzito ambao walisababisha uhaba wa chakula katika eneo hilo.
“Kama serikali, tunatambua hali ya njaa huko Karamoja ambako tunazo ripoti za vifo kutokana na njaa,” msemaji wa waziri mkuu ameiambia AFP siku moja baada ya mkutano na wanasiasa wa eneo hilo.
Ofisi ya waziri mkuu imetangaza kwamba itapeleka tani 200 za msaada na kukusanya dola milioni 36 kununua chakula kwa ajili ya eneo hilo katika miezi mitatu ijayo.