Wafanyakazi wa kutoa msaada wamepata miili 72 ya watu waliofariki kutokana na mafuriko yaliyotokea alhamisi mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Mvua kubwa katika jimbo la Kivu kusini, imesbabisha mito kufurika na kupelekea hasara kubwa wa mali na vifo katika Kijiji cha Bushushu na Ntamukubi.
Gavana wa Kivu kusini amethibitisha ripoti hizo bila kutoa taarisa kamili kuhusu idadi ya vifo.
Idadi kubwa ya waliofariki ni wanawake na Watoto.
Maafisa wamesema kwamba karibu watu 40 hawajulikani walipo.