“Usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi, majambazi waliua watu 7, wanaume wanne na wanawake watatu katika kambi ya waliyohama makazi yao ya Rujagati," Patrick Nkundabera, mkuu wa polisi huko Kashuga, wilaya ya Masisi katika mkoa wa Kivu Kaskazini, ameiambia AFP.
“Waasi wa kundi la Nyatura wanaodhibiti eneo hilo wanashukiwa kufanya shambulio hilo," ameongeza.
Kambi hiyo imeshambuliwa kwa mara ya pili tangu ifunguliwe mwaka wa 2008.
Inahifadhi familia 17,000, wengi ni kutoka jamii ya Wahunde na Wahutu.
DRC ina wakimbizi wa ndani milioni 5.3, kituo kinachofuatilia wakimbizi wa ndani na shirika la Norway linalohudumia wakimbizi walisema katika ripoti yao mwezi uliopita.
Kundi la wanamgambo la Nyatura linaundwa zaidi na raia wa Congo wa kabila la Wahutu, ni mmoja ya makundi mengi yenye silaha yanayoendesha harakati katika eneo hilo.