Watu 6 wauwawa na kombora la Russia, nchini Ukraine

Maafisa wa Ukraine wameripoti mashambulio ya makombora ya Russia ya leo hii katika maeneo mengi ya nchi na kuua takriban watu sita.

Jeshi la Ukraine, limesema kuwa lilitungua makombora 34 kati ya 81 ambayo Russia iliyarusha, na kwamba iliangusha ndege nne zisizo na rubani zilizotengenezwa Iran zinazotumiwa na vikosi vya Russia.

Wavamizi wanaweza tu kuwatisha raia,” Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy aliandika kwenye Telegram.

Hayo tu ndiyo wanaweza kufanya, na haitasaidia” aliongeza kusema.

Rais Zelenskyy alisema maadui zake hawataepuka kuwajibika kwa kila kitu ambacho wamefanya.

Gavana wa eneo la magharibi la Lviv alisema watu watano waliuawa huko baada ya kombora kushambulia eneo la makazi.

Katika mji wa Dnipropetrovsk, maafisa wamesema mashambulizi ya Russia yaliua mtu mmoja na kujeruhi wengine wawili