Watu 6 wafariki katika mlipuko wa bomu Somalia

SOMALIA EXPLOSION

Mlipuko wa bomu uliotekelezwa na waasi wa Kiislamu wenye itikadi kali nchini Somalia ulipiga mgahawa mmoja  maarufu wa kando ya bahari katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu na kuua takriban watu sita, maafisa wa huduma ya gari la wagonjwa wamesema.

Mlipuko huo ulitokea Ijumaa jioni wakati wateja wengi walikusanyika kwa mlo wa futari wakati wa mfungo wa Ramadhani. Mgahawa huo hutembelewa mara kwa mara na maafisa wa serikali.

Waliouawa wengi wao walikuwa raia na watu wengine saba walijeruhiwa, mkurugenzi wa Huduma ya Ambulance ya Aamin, Abdulkadir Adan aliiambia Associated Press kwa njia ya simu. Mlipuko huo ulisababisha "uharibifu mkubwa," alisema.

Kundi la Kiislamu la Al-Shabab nchini Somalia limedai kuhusika na mlipuko huo.