Watu 25 wapoteza maisha kutokana na dhoruba Libya

Magari yanapita kwenye mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha katika mji mkuu wa Libya, Tripoli. Oktoba 19, 2022. Picha na Mahmud TURKIA / AFP.

Wanajeshi saba wa Jeshi la Kitaifa la Libya hawajulikani walipo msemaji wa LNA Ahmad Mesmari alisema.

Dhoruba kubwa ya Mediteranian ilipiga mashariki mwa Libya siku ya Jumapili na Jumatatu, na kuuwa takriban watu 25 na kuharibu nyumba na barabara vyanzo vya afya vilisema.

Wanajeshi saba wa Jeshi la Kitaifa la Libya hawajulikani walipo msemaji wa LNA Ahmad Mesmari alisema.

Picha za kwenye mitandao ya kijamii ziliwaonyesha watu wakiwa wamekwama juu ya mapaa ya magari yao wakati wakijaribu kupata msaada katika mafuriko makubwa wakati kimbunga Daniel kilipopiga miji ya Benghazi, Sousse, Al Bayda, Al-Marj na Derna.

Tulikuwa tumelala, tulipoamka, tulikuta maji yamezingira nyumba. Tuko ndani na tulikuwa tunajaribu kutoka," mkazi wa Derna Ahmed Mohamed aliambia Reuters kwa njia ya simu Jumatatu.