Takriban watu 20 wamewawa na 450 wamejeruhiwa Jumatano katika duru mpya ya milipuko nchini Lebanon, ambapo milipuko ya sasa ikitokea kwenye redio za mawasiliano zilizolipuliwa kwa mbali ambazo hutumiwa na wanamgambo wa Hezbollah.
Moja ya milipuko ilitokea karibu na maziko yaliyoandaliwa na Hezbollah inayoungwa mkono na Iran kwa wanachama watatu wa Hezbollah na mtoto.
Walikuwa miongoni mwa 12 waliouwawa Jumanne wakati maelfu ya vifaa vya mawasiliano vilivyotumiwa na kundi hilo vililipuka kote nchini humo, na kujeruhi takribani watu 3,000.
Hezbollah inalaumu mashambulio yamefanywa na Israel, ambayo haijasema lolote licha ya wataalam wa usalama wa mashariki ya kati na Marekani kuviambia vyombo vya habari vya Marekani kwamba mashambulizi ya Jumanne yalifanywa Mossad, ambayo ni idara ya ujasusi ya Israel.