Raia 18 wameuawa Jumanne mashariki mwa DRC na kundi la kikabila la wanamgambo, ambao walishambulia jengo la kanisa ambako watu waliokimbia ghasia walikuwa wameomba hifadhi, vyanzo vya ndani na makanisa vimesema
Vyanzo hivyo vimesema tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Kilo, katika mkoa wa Ituri.
Afisa wa kanisa katoliki ameliambia shirika la habari la AFP “ Kundi lenye silaha liitwalo CODECO lilitushambulia majira ya saa kumi na moja na nusu alfajiri”.
“Walianza kufyatua silaha zao na sisi tukajificha ndani ya nyumba. Waliingia katika moja ya vyumba kuliko lala watu waliyohama makazi yao. Baada ya kuondoka, tulipata miili 12”.
Jengo hilo la kanisa lilikuwa makazi ya watu 1,000 waliokimbia mauaji katika kijiji jirani cha Matongo, katika wilaya ya Djugu.