Wafanyakazi wa uokoaji nchini Tanzania walifanya kazi ya kuwafikia watu ambao bado wamekwama katika jengo lililoporomoka katika mji mkuu wa kibiashara wa Dar es Salaam leo Jumatatu, huku idadi ya vifo ikiongezeka na kufikia 16.
Shughuli za uokoaji zinaendelea kwa sababu baadhi ya watu bado wamekwama katika jengo hilo, alisema Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa wakati wa ibada ya kuwaombea waathirika. Tunawasiliana na baadhi ya watu waliokwama na kusikia sauti zao, alisema huku akiongeza kwamba watu 86 wameokolewa hadi sasa.
Jengo la ghorofa nne lilianguka Jumamosi katika soko la Kariakoo lenye shughuli nyingi. Majaliwa alisema timu ya wataalamu 19 imeteuliwa kukagua majengo ya ghorofa katika eneo hilo. Haijulikani nini kilichosababisha jengo hilo kuanguka lakini mashuhuda waliviambia vyombo vya habari katika eneo hilo kwamba kulikuwa na ujenzi ulioanza Ijumaa wa kupanua eneo la biashara la chini ya ardhi kwenye jengo hilo.
Tukio hilo limeibua ukosoaji mpya kuhusu ujenzi usiodhibitiwa katika mji huo wa Bahari ya Hindi wenye wakazi zaidi ya milioni tano.