Shirika hilo linasema zaidi ya watu milioni 12 wako hatarini kukabiliwa na ukatili wa kijinsia.
"Watoto wanauawa, wanajeruhiwa, na kuhamishwa, huku ukiukwaji mkubwa wa haki ukiripotiwa kila siku. Wengi wanalazimishwa na kijiunga na makundi yenye silaha, utumwa wa watoto, na ndoa za mapema,” Alisema Lucia Elmi mkurugenzi wa dharura wa UNICEF.
Madhara ya kisaikolojia ni makubwa, mizozo, kupotea na kukabiliana na wasiwasi, upweke pamoja na afya ya akili. Hatua ya dharura inahitajika kulinda watoto wa Sudan.
"Kufikia watoto hawa ni vigumu zaidi. Katika ziara yangu ya hivi karibuni, nilisafiri hadi Kassala, Gedaref na Wad Medani, ambapo nilishuhudia wasichana na wavulana wakichunguzwa kwa utapiamlo, mama wakitafuta matibabu ya dharura kwa ajili ya watoto wao, na familia zikihitaji maji safi na huduma za usafi. Mahitaji ni makubwa, lakini msaada haupatikani kwa kiwango kinachohitajika,” alisema.
"Wakati huo huo, niliona jambo la kushangaza ambapo jamii za wakimbizi na wenyeji walikusanyika pamoja kutoa ujuzi wao na uwezo wao kutoa huduma za kibinadamu; watoto wakitamani kujifunza na kucheza katika vituo vya muda vya kujifunza. Kwa watoto wengi, hii ni fursa yao ya kwanza ya kwenda shule, kwani wanatoka maeneo ambayo hayakuwa na huduma za elimu hapo awali. Vituo hivi si tu kuhusu kujifunza; vinatoa matumaini, na ulinzi. "Pia niliona mabasi, yakiwa yamejaa vitu vichache ambavyo familia ziliweza kubeba, yakielekea maeneo ambapo mapigano yamepungua Seenja, Sennar, na Wad Madani.
Wazazi wanachukuwa tahadhari kuanza safari ya kurudi nyumbani, wakitumaini hali itakuwa thabiti ili waweze kujenga upya maisha yao. Lakini pia nilikutana na familia ambazo hazina nyumba ya kurudi. Vijiji vyao vimetoweka, jamii zao zimevunjika. Wamekwama na hawana matumaini kwa ajili ya kesho. "Utoaji wa msaada wa kibinadamu unaendelea kukwama kutokana na vikwazo vya kiserikali na kiutawala katika kupata vibali vinavyohitajika kwa utoaji wa vifaa katika maeneo yaliyokumbwa na mizozo ya silaha.
Mapigano yanayoendelea, ukatili unaotokana na vita vya kikabila, na mashambulizi ya moja kwa moja kwa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu na vikundi vya msaada vinafanya hali kuwa mbaya zaidi. Wizi na ukatili vimefanya kusitishwa kwa shughuli katika maeneo mengi. "Mwaka jana, shida ya chakula Sudan iligeuka kuwa njaa, jambo ambalo tulikuwa tukionya kwa muda mrefu, na sasa tunatabiri kuwa hali inazidi kuwa mbaya. Tangu Aprili 2023, idadi ya watu wanaokumbwa na uhaba wa chakula imeongezeka mara tatu. Hali ya njaa inatokea angalau maeneo matano, ikiwemo kambi za wakimbizi kaskazini mwa Darfur na Milima ya Nuba Magharibi. "Kitaifa, watoto milioni 3.2 walio na umri wa chini ya miaka mitano wanatarajiwa kukabiliwa na utapiamlo mwaka huu, ikiwemo 770,000 ambao tarayi wana utapiamlo.
Katika maeneo yaliyoathiriwa na njaa, huduma za kimsingi zimeshindwa kufinka .
"Licha ya changamoto kubwa, UNICEF inaendelea na jitihada za kusaida. Katika mwaka 2024, tulifanikiwa: Kutoa msaada wa kisaikolojia, elimu, na huduma za ulinzi kwa watoto milioni 2.7 na wale wanaowatunza. Kutoa maji salama kwa watu milioni 9.8. Kuchunguza watoto milioni 6.7 kwa utapiamlo na kutoa matibabu ya kuokoa maisha kwa watoto 422,000. Mnamo mwaka 2025, tutaendelea kutoa msaada wa dharura huku tukifanya kazi kurejesha huduma muhimu na kujenga ustahimilivu katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi,” alisema.
"Sudan inakabiliwa na hatari ya kupoteza kizazi kizima. Tunatoa wito kwa wahusika wote serikali, wahisani, na pande zote za mzozo kuchukua hatua sasa: Hakikisha upatikanaji wa misaada ya kibinadamu kupitia mistari ya mizozo na mipaka. Linda wafanyakazi wa kibinadamu na vifaa vya msaada. Ongeza ufadhili ili kukabiliana na mahitaji yanayoongezeka. Lidisha ukatili. "Watoto wa Sudan hawawezi kusubiri. Dunia lazima ichukue hatua—sasa."