Watetezi wa haki za binadamu wana wasiwasi n uchaguzi wa Pakistan

Makundi ya haki za binadamu, na waangalizi wa kujitegemea nchini Pakistan, wameelezea matumaini yao Jumatatu kuhusu haki na kuaminika kwa uchaguzi wa bunge wa Februari 8.

Kwa upande mwengine yamegusia namna serekali inayoungwa mkono na jeshi inavyofuatilia vyama vya siasa vyenye ufuasi mkubwa na kuongezeka kwa udhibiti wa vyombo vya habari.

Kusakwa huko kumemlenga waziri mkuu wa zamani aliyefungwa Imran Khan wa chama cha Tahreek-e-Insaf, ama PTI, kinacho elezwa kuwa chama kikubwa cha kisiasa kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni.

Munizae Jahangir, mwenyekiti mwenza wa tume huru ya haki za binadamu ameuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Islamabad, kwamba mpaka wakati huu kuna ushahidi mdogo kwamba uchaguzi ujao utakuwa huru, wa haki ama kuaminika.