Watetezi wa haki za binadamu waikosoa Pakistan

Watetezi wa haki za binadamu wameikosoa vikali Pakistan kwa kutangaza mipango ya kutumia sheria za kijeshi kuwafungulia mashtaka waliohusika na uchomaji moto wakati wa maandamano ya hivi karibuni yaliyotokana na kukamatwa kwa waziri mkuu wa zamani Imran Khan.

Katika taarifa yake siku ya Jumanne, Amnesty International ilielezea hatua hiyo yenye utata kuwa ya kutisha na kinyume cha sheria za kimataifa, na kutaka iondolewe mara moja.

“Hii ni mbinu ya vitisho iliyoundwa ili kukabiliana na upinzani kwa kuogopa taasisi ambayo haijawahi kuwajibishwa kwa unyanyasaji wake,” amesema Dinushika Dissanayake, naibu mkurugenzi wa Amnesty International kanda ya Asia Kusini, akimaanisha watu wenye uwezo mkubwa yaani jeshi la Pakistan.

Khan alichukuliwa kwa nguvu na kukamatwa na vikosi vya kijeshi kwa mashitaka ya ubadhirifu kutoka nje ya mahakama katika mji mkuu wa Islamabad, wiki iliyopita wakati akijiandaa kusikiliza keshi nyingine tofauti.