Watanzania wasubiri kwa hamu matokeo ya uchaguzi mkuu

  • Abdushakur Aboud

Msimamizi wa kituo cha kupiga kura akitayarisha vifaa vya uchaguzi huku watu wakisubiri kufunguliwa kituo ili waweze kupiga kura

Watanzania wanasubiri kwa hamu kusikia matokeo ya uchaguzi mkuu ulofanyika Jumapili Oktoba 31 kwa amani na utulivu.

Khadija Riyami mwandishi wa Sauti ya Amerika huko Dar es Salaam alieleza asubuhi ya Jumatatu kwamba mashindano yalikua makali na tume ya uchaguzi imesema haitoweza kutangaza matokeo ya awali hadi hapo saa tano mchana saa za Tanzania.

Anasema mfano mmoja katika kituo cha Busanda huko Mwanza "wamehesabu kura wamemaliza imeonekana kwamba mgombea wa Chadema alipata kura nyingi sana, lakini mpaka asubuhi haikueleweka matokeo kwani wakala wa Chadema alitoka kwenye chumba cha kuhesabu akiwa na furaha kama aliyepatwa na kiwewe".

Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam hakuona jina lake

Baada ya hapo tena anasema watu walokua nje walingia ndani wakafanya fujo na kuwapiga mawakala wawili wwalojeruhiwa na kupelekwa hospitali. sasa haieleweki nini kilichotokea.

Huko Zanzibar inaripotiwa kura zinaendelea kuhesabiwa na baada ya kuhesabiwa kwa wilaya 15 mgombea wa chama tawala CCM, Ali Mohamed Shein alikua anaongoza mbele ya mgombea wa chama cha Cuf, Maalim Seif Sharif lakini hapo baado kura za Pembe na sehemu nyingine za Unguja kuhesabiwa.

Kwa ujumla wafuatiliaji wa kimataifa wanasema upigaji kura ulikwenda shwari na kwa mpangilio, wakiripoti kwamba baadhi ya vituo vya kupigia kura vilichelewa kufunguliwa na kulikuwepo na baadhi ya malalamiko kutokana na kutokuwepo na majina ya baadhi ya wapigaji kura katika orodha ya wapiga kura.