Wanamgambo wenye uhusiano na kundi la kigaidi la al Qaida wamedai kuhusika na sh,ambulizi hilo. Mlipuko huo pia umewajeruhi watu wengine 14 pamoja na kuharibu majengo mengine karibu na mgahawa huo kwenye mji wa Jowhar ulioko takriban kilomita 90 kaskazini mwa mji mkuu wa Mogadishu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, washambuliaji waliendesha gari lililojaa vilipuzi kwenye ukuta wa mgahawa wa Nur-doop, ambao ni maarufu sana miongoni mwa wabunge pamoja na maafisa wa serikali. Afisa wa usalama Mohamed Ali kutoka mjini humo alisema kwamba miongoni mwa watu waliokufa ni wanawake waliokuwa wakifanya kazi kwenye mgahawa huo.
Waziri mkuu mpya Hamza Abdi Barre aliyeidhinishwa na bunge mwezi Juni ametuma salaam za rambi rambi kwa waathirika huku akiahidi msaada wa serikali kwa wale waliojeruhiwa kwenye mkasa huo.