Watalaam wa uchaguzi kutoka nje wamewasili katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kuongelea uwezekano wa kuangalia upya uchaguzi uliopingwa wa Congo.
Shirika moja lenye makao yake Marekani National Democratic Institute na taasisi ya kimataifa ya mifumo ya uchaguzi wamesema wamepeleka timu huko Congo kwa ombi la wanasiasa wa nchini humo.
Waangalizi wa kimataifa wamesema kura hiyo ilikuwa na kasoro kubwa hasa katika hatua ya kuhesabu ambayo waangalizi wameita vurugu.
Wataalam hao walianza mikutano na maafisa wa Congo alhamisi katika mji mkuu, Kinshasa. Taarifa hiyo inasema timu hiyo itaangalia nyaraka za uchaguzi na taarifa, na kuongea na maafisa wakuu kuangalia kama tathmini kubwa zaidi inaweza kuhakiki matokeo .
Tume ya uchaguzi ilimthibitisha rais Joseph Kabila kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais , matokeo ambayo wapinzani wake waliyakataa kwasababu ya tuhuma za wizi.