Wataalamu wa sera za kigeni wanatofautiana kuhusu mwelekeo wa sera ya Marekani kwa Ukraine, endapo Donald Trump atarejea White House, utabiri ukiwa ni kuanzia katika uungwaji mkono mkubwa zaidi wa Marekani, hadi shinikizo kubwa kwa Kyiv kukubali ardhi yote ambayo tayari imepoteza.
Iwapo Biden, atashinda tena uchaguzi huo, wengi wanasema, sera ya Ukraine haito badilika, kukiwa na uwezekano wa vikwazo vikali zaidi kwa Russia.
Msimamo wa Trump juu ya Ukraine na vita vya Russia, haupo wazi na usio eleweka.
Februari 22, 2022, siku mbili tu kabla ya Russia, kuanzisha uvamizi wake kamili wa Ukraine, Trump alitaja hatua za Rais wa Russia, Vladimir Putin dhidi ya Ukraine kuwa yenye ujuzi na fikra.
Mwaka uliofuata wakati wa kipindi maalumu cha televisheni ya CNN, Trump alikataa kueleza upande gani anataka ushinde Ukraine, ama kuahidi kuhakikisha Ukraine inapata msaada wa zaidi wa kijeshi.