Wataalam wa afya ya akili watumwa Hawaii kuwasaidia wakazi waliokumbwa na mkasa wa moto

Timu za waokozi zikitafuta manusura kwenye mabaki ya gari zilizochomeka Maui, Hawaii

Wataalamu wa afya ya akili wanaendelea kuwasaidia wakazi wa kisiwa cha Maui, jimbo la Hawaii, hapa Marekani, walionusurika na moto mbaya unaoendelea kuwaka baada ya zaidi ya karne moja, kukabiliana na maisha baada ya mkasa huo.

Watu wengi wao bado wakiwa katika hali ya mshtuko, baadhi wameelemewa na msongo wa mawazo na kiwewe, hali ambayo wataalam wanasema huenda ikachukua muda mrefu kuondoka.

Anne Landon mwenye umri wa miaka 70 mkazi wa kisiwa hicho mara mbili amekwenda kwenye kituo maalum kilichofunguliwa, ili kupata msaada wa kisaikolojia na huduma nyingine za kumsaidia.

Mmoja wa wataalam aliozungumza nao alimfundisha namna ya kupumua ili kupunguza kasi ya mapigo ya moyo. Na pia wakati mwingine alimpata muuguzi aliyekuwa anahudumia watu kwa saa 24 kwenye hifadhi ambay alimliwaza alipokuwa akilia.

Landon anasema kwamba imekuwa vigumu kwake kuwasiliana na watu, na hata baada ya kupata huduma za internet, bado ameshindwa kuwasiliana na watu hata wale ambao wamekuwa wakimtumia ujumbe.