Mwaka huu kuna matumaini kwamba tani 30,000 za ngano kutoka nchi nyingine iliyokumbwa na vita, Ukraine, zitapunguza njaa kwa baadhi ya Waafghanistan. Umoja wa Mataifa unasema njaa iko karibu kote nchini Afghanistan huku asilimia 97 ya watu wake sasa wakiishi chini ya mstari wa orodha ya umaskini.
“Licha ya mateso yake katika kukabiliana na uvamizi wa kikatili wa Russia Ukraine imetoa tani 30,000 za nafaka kupitia WFP ili kupunguza mzozo wa kibinadamu wa Afghanistan," Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, aliandika kwenye Twitter mwezi uliopita.
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani linasema ngano hiyo inasagwa kuwa unga nchini Uturuki na kisha kusafirishwa hadi Pakistani ambako itapelekwa Afghanistan kwa malori.