Washington yatangaza mkakati wake wa kimataifa kupambana na ugaidi Afrika

Your browser doesn’t support HTML5

Makundi ya kigaidi barani Afrika kama vile al-Shabaab ya Somalia, Boko Haramu nchini Nigeria yanayo sababisha ghasia katika baadhi ya sehemu ya bara hilo.

Washington ilitangaza mwezi Agosti mkakati wake mpya kwa ajili ya nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara kupambana na vitisho vya makundi hayo ya kigaidi dhidi ya maslahi ya Marekani na washirika wake.

White House imesema itafanya kazi na nchi za Kiafrika kwa misingi ya nchi kwa nchi na ya kikanda ili kufikia malengo ya pamoja. Sikiliza repoti kamili...