Wakazi wa Nouna, mji wa mkoa wa Kossi magharibi mwa nchi, walioawasiliana kwa simu na shirika la habari la AFP, wamesema mji huo ulishambuliwa kwa makombora Jumatatu jioni.
Mkazi mmoja amesema “watu sita walikufa na wanne kujeruhiwa.”
Mji wa Nouna ulipokea katika miezi ya karibuni maelfu ya watu waliokimbia mashambulizi ya mara kwa mara ya wanamgambo wa kiislamu kwenye makazi yao.
Chanzo cha usalama kimeithibitishia AFP shambulio la Nouna, na kusema “mabaki ya roketi yalipatikana katika eneo hilo.”
Jioni hiyo hiyo, kwenye umbali wa kilomita 400 kusini mwa nchi, mji wa Tondoura ulio karibu na mpaka wa Ivory Coast, ulishambuliwa pia, chanzo kimoja ambacho hakikutaka jina lake litajwe kimeiambia AFP.
Chanzo hicho kimesema” magaidi walishambulia kijiji. Baadhi ya wanakijiji, wakiwa na bunduki, walijaribu kuingilia kati lakini walivamiwa haraka.”