Warepublikan 9 watangaza kugombania uspika

Wawakilishi tisa wa chama cha Republican, Marekani, katika baraza la wawakilishi, ambao wote hawafahamiki vyema na umma wa Marekani, wametangaza Jumapili ambayo ni siku ya mwisho kutaka kugombea uspika.

Bunge hilo limekuwa bila spika kwa takriban wiki tatu baada ya wabunge wanane wa upande wa mrengo mkali wa kulia wa chama cha Republican kuungana na Wanademokrat wote 212 katika baraza hilo la wawakilishi kumtimua aliyekuwa spika wa wakati huo Kevin McCarthy.

Kikundi hicho kidogo cha Warepublican kilikasirishwa kwamba McCarthy alikubali mpango wa matumizi ya serikali na rais wa Mdemokrat, wa Marekani, Joe Biden, ambao walihisi kuwa ni mkubwa sana kuzuia kufungwa kwa sehemu ya serikali na kuwezesha shughuli za serikali kufadhiliwa hadi Novemba 17.