Warepublican wanakosoa uamuzi wa Trump kutoa msamaha kwa Arpaio

Spika wa bunge la Marekani, Paul Ryan.

Spika wa bunge la Marekani, Paul Ryan alisema hakubaliani na uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kutoa msamaha kwa Joe Arpaio, Sheriff wa zamani katika jimbo la Arizona ikiwa ni chini ya mwezi mmoja baada ya kukutwa na hatia ya uhalifu katika kesi iliyohusisha idara yake katika sera za ubaguzi.

Maafisa wa idara ya polisi wana wajibu maalumu wa kuheshimu haki ya kila mtu nchini Marekani. Tusiruhusu mtu yeyote kuamini kwamba uwajibikaji umefutwa na msamaha huu, msemaji wa Ryan, Doug Andres alisema katika taarifa hiyo.

Wote maseneta wa chama cha Republican kutoka jimbo la Arizona, John McCain na Jeff Flake pia walikosoa hatua hiyo iliyofanywa na Rais Trump.