Uchaguzi wa bunge wa Iran wasusiwa na upinzani

Kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei akipiga kura yake kwenye uchaguzi wa bunge wa Ijumma mjini Tehran.

Uchaguzi wa bunge wa Iran Ijumaa umeonekana kuwa mtihani mkubwa kwenye uhalali wa taifa hilo la kidini, baada ya idadi ndogo ya asilimia 40 kujitokeza kulingana na taarifa zisizo rasmi kutoka kwa vyombo vya habari.

Watu wenye msimamo wa kati pamoja na wakonsavative wanasemekana kususia zoezi hilo, wakati wanaharakati wa mabadiliko wakisema kuwa haukua huru na wenye haki kwa kuwa ulionekana kuwa ushindani kati ya wenye misimamo mikali na wakonsavative wanaounga mkono misimamo ya kiislamu.

Mohammad Khatami ambaye alikuwa rais wa kwanza wa mageuzi nchini humo alikuwa miongoni mwa wale waliosusia kura hiyo. Mshindi wa tuzo ya Nobel wa Iran, Narges Mohammadi aliyefungwa jela, na ambaye pia ni mwanaharakati wa haki za wanawake, kupitia taarifa iliotolewa na familia yake amesema kwamba uchaguzi huo ulikuwa feki.