Rais aliye madarakani Ali Bongo anawania muhula wa tatu. Ameiongoza nchi hiyo tangu mwaka 2009. Kabla ya hapo, baba yake aliliongoza taifa hilo la Afrika ya Kati lenye utajiri wa mafuta.
Albert Ondo Ossa, mmoja kati ya wagombea 14 wa urais amesema “Gabon sio mali ya kina Bongo.”
Ondo Ossa mgombea wa muungano mkuu wa vyama vya upinzani, Alternance 2023 aliteuliwa wiki iliyopita.
Mabadiliko ya hivi karibuni kwenye sheria ya upigaji kura mwaka huu imebainika kuwa yenye utata, huku wakosoaji wakisema hatua mpya inakinufaisha zaidi chama tawala cha Gabonese Democratic.
Kutokana na mabadiliko hayo, kura kwa naibu kiongozi wa manispaa itakuwa mara moja kura kwa naibu mgombea urais.
Wakosoaji wanasema kwamba mabadiliko hayo yatafanya uchaguzi usiwe wa haki, kwa sababu mgombea wa upinzani Ossa haungwi mkono na chama kimoja pekee.