Kwa mujibu wa repoti iliyotolewa na shirika la uhakiki wa wapiga kura, KPMG, idadi hii huwa muhimu hasa wakati wa kinyang’anyiro cha uchaguzi wenye ushindani mkali.
Hili pia linatoa mwanya kwa wizi wa kura, jambo ambalo limeelezwa kuwa moja ya mapungufu yaligubika matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2007.
Mgogoro kama huu ndio uliosababisha uvunjifu wa amani na kusababisha vifo vya watu 1,133.
Suala la wapiga kura walio kwisha kufa” wakifufuka siku ya kupiga kura kuchagua wagombea” limeleta ugomvi mkubwa siku za nyuma, wakati wanasiasa wakisema kuwa lilitoa fursa kwa wizi wa kura kufanyika.
Kwa mujibu wa uhakiki, ambao matokeo yake yaliwasilishwa kwenye tume ya uchaguzi leo, kuna uwezekano wa kuwepo wapiga kura hewa 1,037,260 katika daftari la usajili ambao walishakufa tangu Novemba 2012 na Disemba mwaka jana,
Kwa kulinganisha takwimu zilizoko katika daftari kuu la usajili wa uzazi na vifo, uhakiki huo umegundua kuwa kulikuwa na watu 435,157 ambao tayari walikuwa wamethibishwa kufa kwao lakini bado majina yao yalikuwa katika daftari la usajili.
Kwa mujibu wa uhakiki huo usajili unaofanya kupitia kifaa cha biometric kielektroniki ndio unapaswa kuwa ni njia ya msingi katika kuwatambua wapiga kura wakati wa uchaguzi. Kwa sababu ikiwa utaratibu huu haufuatwi kuna uwezekano mkubwa watu waliokuwa wameshakufa kuhusishwa na uchaguzi.