Wapalestina wakagua uharibifu wa majengo Gaza City

Picha za uharibifu wa majengo Gaza.

Wapalestina wakagua uharibifu wa majengo Gaza City.

Wapalestina wanakagua uharibifu wa majengo Gaza City kufuatia shambulizi la Israel lililouwa watu kadhaa, kwa mujibu wa wizara ya afya.

Mahmoud Al- Ghafry anayeishi karibu na eneo hilo amesema juhudi zinaendelea kuwapata watu waliokwama katika vifusi.

Huko Gaza , wafanyakazi wa afya wanasema takriban wapalestina 13 waliuwawa usiku katika mashambulizi tofauti ya Israel ikiwemo katika nyumba mbili Gaza City na kwenye kambi moja .

Israel imefanya shambulizi la anga na la ardhini Gaza baada ya wapiganaji wanaoongozwa na Hamas kuvamia jumuiya za Israel miezi 14 iliyopita na kuuwa watu 1,200 na kuwashikilia mateka wengine 250, kwa mujibu wa hesabu za Israel.

Israel imesema takriban mateka 100 bado wanashikiliwa lakini haijulikani ni wangapi bado wako hai.