15 waokolewa katika ajali ya ndege

Picha ya maktaba ya ajali ya ndege iliyotokea nchini Taiwan, mwaka 2014 ya shirika la TransAsia.

Wafanyakazi wa uokozi nchini Taiwan, wametumia “crane” kuinua sehemu ya mabaki ya ndege ya abiria iliyoanguka Jumatano, nje ya mji wa Taipei.

Ajali hiyo mpaka sasa imeua watu karibu 25, na kuacha wengine 20 wakipotea katika mto wenye kina kidogo.

Ndege hiyo aina ya ATR-72 iligusa daraja kwa bawa lake moja na kudondokea katika mto Keelung mara baada ya kuruka aiku ya Jumatao.

Picha na video zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii, zinaonyesha ndege hiyo katika nyuzi 90, na kwa kiwango kidogo ilikosa kugonga magorofa marefu ambayo ni makazi ya watu.

Boti za uokozi zilizunguka ndege hiyo iliyokuwa imeanguka juu chini na kuwatoa abiria 15 kwenye usalama akiwemo mtoto.

Mkurugenzi wa shirika la TransAsia, Chen Xinde, baadaye alitoa rambi rambi zake na kuomba radhi kufuatia ajali hiyo katika mkutano na wanahabari.