Watu wenye silaha nchini Nigeria, wamewateka watu wanne kutoka nyumba moja katika mji wa chuo kikuu cha Keffi, katikati mwa jimbo la Nasarawa, polisi wamesema Jumanne.
Utekaji nyara ili kulipwa fidia umekithiri nchini Nigeria, lakini mashambulizi mengi yamekuwa katika eneo la kaskazini magharibi ambako watu wenye silaha wamewalenga wanafunzi wa chuo kikuu.
Msemaji wa polisi wa Nasarawa, Rahman Nansel alisema polisi walipokea simu ya saa 8:55 Jumanne, usiku baada ya watu wenye silaha kuvamia nyumba ya jamii ya watu wa Angwan Kaare.
Amesema polisi walifika pamoja na wanajeshi, lakini watekaji hao tayari walikuwa wamekimbia na wale waliotekwa.
“Kamishna wa Polisi ameamuru msako wa wahalifu kwa nia ya kuwaokoa watu wanne waliotekwa wakiwa salama.
Keffi inapatikana takriban kilomita 70 mashariki mwa Abuja, mji mkuu wa Nigeria.