Wanawake wameweka historia katika uchaguzi mkuu Kenya

Wanawake wakishiriki maandamano ya kutaka haki na usawa kwa wanawake katika jamii yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya. Nov. 17, 2014.

Kati ya wagombea wanne wenza katika uchaguzi wa rais wa wiki ijayo nchini Kenya, wagombea watatu ni wanawake, akiwemo mgombea mwenza wa Raila Odinga.

Uchaguzi huenda ukabadili siasa za Kenya. Lakini wanawake wanasiasa wanasema kufikia katika hatua hii ya historia imekuwa si kazi rahisi.

Haijawahi kutokea nchini Kenya. Wagombea watatu kati ya wanne wanaowania nafasi za naibu rais katika uchaguzi wa Agosti 9 ni wanawake.

Wakusanyaji maoni wanasema waziri mkuu wa zamani Raila Odinga na mgombea mwenza wake waziri wa zamani wa sheria Martha Karua wanaongoza katika kundi hilo la wagombea urais kabla ya upigaji wa wiki ijayo.

Ushawishi wa wanawake katika kura za urais

Mchambuzi na mtafiti wa siasa, Tom Wolf anasema “Unapokuwa na mwanamke maarufu kama Martha karua ambaye alikuwa mbunge kwa miaka 15 au 20, alihudumu katika baraza la mawaziri la Mwai Kibaki, na akaondoka kwa sababu maalum za kimaadili amekuwa kiongozi wa chama cha siara cha Nark Kenya. Nadhani hiyo imefanya iwe rahisi kwa wagombea wengine wawili wa urais kuona ni sawa kuwa na mwanamke. Na pengine kisiasa ni fursa nzuri kuwa na mwanamke mgombea mwenza.”

Justina Wamae – mgombea mwenza wa Prof Wajackoya

Justina Wamae anawania ugombea mwenza na mgombea urais Profesa George Wajackoyah. Alikulia akiwaangalia wanawake wanasiasa kama Martha Karua ambaye ni mshindani wake hivi sasa.

“Nina furaha kwasababu Martha Karua na wanawake wengine kama Mama Ngilu, walivunja dar ya kioo. Hivi sasa wameiacha wazi. Kwa sisi watatu ni jambo kubwa sana,” anasema Justina Wamae wa mgombea mwenza kwa tiketi ya chama cha Roots.

Chama chake cha Roots Party kimekuja na ilani ya uchgui ambayo haikutarajiwa nchini Kenya ikiahidi kuwanyonga wale ambao watakuwa na hatia ya rushwa, wiki ya kazi kuwa ni siku nne, na kuhalalisha bhangi.

“Profesa George Wajackoyah na mimi tuna mtizamo. Tunawaambia kwamba tunataka kuhalalisha bhangi kwasababu wa kuchochea uchumi. Lengo letu ni kwamba hatutaongeza kodi, tutalipa madeni na tutaachana na kutegemea ufadhili kwasababu nchi hii lazima iheshimiwe,” anaelezea zaidi Justina.

Ruth Mutua, mgombea mwenza wa David Mwaure

Wakati huo, Ruth Mutua ni mgombea mwena wa chama cha Agano ambapo mgombea urais ni David Waihiga.

Baadhi ya wakenya wanasema jukumu la wanawake limeingizwa katika siasa, wakati wengine wanasema wanawake hatimaye wanatambuliwa kwa kazi yao katika nyanja ambazo zimetawaliwa na wanaume.

Maoni ya wakenya kuhusu wagombea wenza wanawake

Julie Kisaina, Mkaazi wa Nairobi anasema jinsi hali ilivyokuwa katika suala la wagombea wanawake.

“Tulikuwa tukiambiwa kwamba wanaume wanatakiwa kuitawala jamii. Walitakiwa kutongoza. Lakini hivi sasa kila mtu anatambua kwamba tunaweza kufanya kama wanachofanya wanaume na kufungua uwanja wa kujielezea weneywe na pia kusaidia katika uongozi. Ni vizuri sana.”

Mtazamo wa wachambuzi wa siasa za Kenya

Wanawake wawili walishindwa katika juhudi zao za awali kuwania nafasi ya juu ya uongozi nchini Kenya. Wachambuzi wa siasa wanasema uchaguzi huu huenda ukaonyesha kwa mara wa kwanza mwanamke naye anashika nafasi ya juu katika siasa za Kenya yaani wadhifa wa naibu rais.