Wanasiasa wa Upinzani nchini Venezuela wameungana dhidi ya chama kinachotawala

Rais wa Venezuela Nicholas Maduro (kulia) akiwa na generali mstaafu Hugo Carvajal wakati wa mkutano wa chama cha kisoshalisti mjini Caracas July 27, 2014

Rais wa Venezuela Nicholas Maduro (kulia) akiwa na generali mstaafu Hugo Carvajal wakati wa mkutano wa chama cha kisoshalisti mjini Caracas July 27, 2014

Wanasiasa wa upinzani wataandaa uchaguzi jumapili, kumtafuta mgombea mmoja kuwakilisha katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao 2024 licha ya mgombea anayeonekana kuwa na ufuasi mkubwa kuzuiwa kugombea urais.

Uchaguzi huo wa vyama vya upinzani kumtafuta kinara mmoja, ni wa kwanza kwa vyama hivyo kuandaliwa katika muda wa miaka 11.

Serikali na upinzani wamesaini taarifa ya pamoja inayosema kwamba kwamba kila upande upo huru kuchagua kinara wake kulingana na sheria zao za chama.

Huenda hii ikawa fursa nzuri kwa wanasaisa wa upinzani kuwashawishi wafuasi wake, katika nchi hiyo inayopitia hali ngumu ya uchumi kwa miaka kadhaa.

Maria Corina Machado, anayetarajiwa kushinda tiketi ya upinzani amepigwa marufuku kugombea urais tangu mwezi Juni, kwa sababu aliunga mkono vikwazo vya Marekani dhidi ya utawala wa rais Nicholas Maduro, na kumuunga mkono kiongozi wa upinzani Juan Guaido. Wagombea wengine wawili, kati ya 12 waliosajiliwa kugombea nafasi hiyo, wamejiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho.